Pep Guardiola amewaengua baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha Manchester City kufanya mazoezi na wengine kufuatia kuongezeka uzito kupita kiasi.
Awali, iliarifiwa kuwa Yaya Toure na Samir Nasri walikuwa wahusika wakuu katika suala hili ili kuwafanya warudi katika hali yao ya kawaida.
Japokuwa hakutaja mtu yeyote, beki wa kushoto wa klabu hiyo Gael Clichy ametanabaisha kwamba kuna baadhi ya wachezaji ambao kocha aliwaengua mpaka pale timu ilipokwenda nchini China.
Clichy amesema kwamba, Man City chini ya utawaka wa Guardiola, mambo yamebadilika na kuwa tofauti kabisa na hapo awali.
“Ndani ya uwanja, nje ya uwanja, kila kitu kinachukuliwa kwa umakini,” Clichy aliwaambia waandishi. Kwa mfano, mara nyingi unasikia mameneja wakisema kuwa na afya bora ni muhimu. Sasa kwake yeye, kama uzito wako ni mkubwa sana, basi haufanyi mazoezi na timu.
“Hiko ndicho kitu cha kwanza na nimekuwa nikisikia mara nyingi sana lakini kwangu mimi ni mara ya kwanza kuona meneja akifanya hivyo. Hivyo tuna wachezaji wachache ambao bado hawafanyi mazoezi na timu, ni suala la kufurahisha kidogo, lakini sisi tunacheza soka na ni ndio kazi yetu na pia tunapaswa kuwajibika kwa kile tunachokifanya uwanjani.”
Bila shaka unaweza kuwa na ubora lakini unapaswa kujua kwamba kama uzito wako ni kilo 60 halafu uko kwenye kilo 70, basi hauwezi kucheza mpira kwasababu utapata majeraha na kuiweka timu yako katika wakati mgumu.”
Guardiola pia amegusia juu ya mpango mpya wa chakula kwa wachezaji wake, hasa piza, chakula ambacho kimekuwa kikitumiwa na wachezaji wa timu yake baada ya mechi katika miaka ya hivi karibuni na vitu vingine sasa vimepigwa marufuku.
“Amepiga marufuku baadhi ya juisi na bila shaka piza na vitu vyakula vyote vizito-vizito haviruhusiwi,” Clichy aliongeza. “Ni kitu cha kawaida lakini watu wengine wanadhani kwamba, ni kawaida mno, ingetakiwa kuwa hivi, lakini kiukweli sio kila kitu kunakuwa kama hivi na najua kwasababu nimekuwa nikicheza soka kwa muda mrefu sasa. Inasisimua kwa kweli.”
Wachezaji wengi ambao walikuwa kwenye timu zao za taifa, wameungana na wenzao katika kikosi cha Manchester City nchini China, lakini Clichy anasema kwamba wapo pale kwa geresha lakini watakuwa fiti zaidi watakaporejea England.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment